1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yahujumu maficho ya waasi Sudan

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClYl

NDJAMENA:

Ndege za kivita za Chad zimeshambulia ngome ya waasi wanaoipinga serikali ya Ndjamena.

Kambi za waasi hao zinapatikana kusini magharibi mwa El-Geneina katika mkoa wa Darfur nchini Sudan. Duru za kijeshi zinasema shambulio hilo lilifanywa na ndege mbili aina ya helikopta.

Waasi wana kambi kadhaa kilomita 200 kutoka mji wa jangwani wa Chad unaoitwa Abeche.