1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CEBU: Viongozi wa mataifa ya Kusini Mashariki mwa bara la Eshia waanza kikao nchini Philippines.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCb3
Kansela Angela Merkel ,waziri wa mambo ya nchi za nje Steinmeier na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Barroso
Kansela Angela Merkel ,waziri wa mambo ya nchi za nje Steinmeier na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya BarrosoPicha: AP

Viongozi wa Umoja wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Bara la Eshia wameanza mkutano wao wa kila mwaka katika kisiwa cha Cebu nchini Philippines.

Kikao hicho ambacho kimeekewa ulinzi mkali ni cha kumi na mbili kuandaliwa katika muda wa miaka arobaini tangu Umoja wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Eshia ulipoundwa.

Mataifa yote kumi wanachama wa Umoja huo yamekubaliana kuwa na eneo la biashara uhuru kufikia mwaka elfu mbili na kumi na tano.

Kikao hicho kiliahirishwa mwezi Disemba baada ya mataifa kadhaa ikiwemo Marekani, Australia, na Uingereza kutahadharisha uwezekano wa kutukia shambulio la kigaidi.

Umoja huo unajumuisha Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos, Malaysia, Burma, Philippines, Singapore, Thailand na Vietnam.