1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CEBU: Viongozi wa Eshia Kusini Mashariki wajadiliana jinsi ya kukabiliana na ugaidi.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbg

Wakuu wa mataifa ya eneo la kusini mashariki mwa Eshia wanakutana nchini Philippines kwa mkutano wa kimkoa siku moja baada ya nchi hiyo kukabiliwa na miripuko ya mabomu.

Mataifa hayo yanakutakana kujadiliana jinsi ya kukabiliana na ugaidi na pia kuhusu ushirikiano wa kiuchumi.

Miripuko ya mabomu ilitokea jana katika eneo la kusini la nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu saba.

Hata hivyo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Philippines ALBERTO Romulo alisema mkutano huo unaofanyiwa katika kisiwa cha Cebu utaendelea kama ulivyokuwa umepangwa.

Hata kabla ya miripuko hiyo, hali ya usalama kisiwani humo ilikuwa imedhibitiwa.

Mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanywa mwezi Disemba lakini ukaahirishwa baada ya kimbunga kupiga katika eneo hilo.