CDU cha Merkel chapata pigo katika uchaguzi wa majimbo | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CDU cha Merkel chapata pigo katika uchaguzi wa majimbo

HESSEN:

Chama cha Kansela wa Ujerumani-Angela Merkel- cha Christian Democratic Union –CDU- kimepoteza uchaguzi katika mikoa miwili.Katika mkoa wa Hesse,CDU kikiongozwa na mkuu wa jimbo hilo Roland Koch,kilipata asili mia 36.8 ya kura ambayo ni chini ya asili mia 49 kilichopata mwaka wa 2003.Hata hivyo asili mia hiyo ni tosha kukifanya CDU kubaki chama chenye nguvu ingawa kwa kiasi kidogo.

Chama cha Social Democrats-kikiongozwa na Andrea Ypsilanti kilipata kura asili mia 36.7.Haijulikani ikiwa chama cha CDU kitabaki madarakani katika mkoa huo.Na kwa mda huohuo katika Lower Saxony,CDU chini ya uongozi wa Christian Wulff- kimerejeshwa madarakani baada ya kupata asili mia 43 ya kura.Asili mia hiyo ni ya chini kutoka asili mia 48 kilichopata mwaka wa 2003.Hata hivyo asili mia hiyo ni tosha kwa CDU kuweza kuunda serikali na chama kingine cha FDP katika mkoa huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com