CARACAS:Hugo Chavez asifu kujiuzulu kwa Rumsfeld waziri wa ulinzi wa Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CARACAS:Hugo Chavez asifu kujiuzulu kwa Rumsfeld waziri wa ulinzi wa Marekani

Rais wa Venezuela Hugo Chavez amesifu uamuzi wa kujiuzulu waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld akisema hata rais Bush anastahili kujiuzulu.

Chavez amesema ushindi wa chama cha Demokratic ni dhihirisho tosha kwamba uchaguzi huo ulikuwa ni adhabu dhidi ya sera za rais bush na vita nchini Iraq.

Chavez akizungumza na waandishi wa habari wa kigeni nchini mwake amesema huu ni mwanzo wa kuanguka kwa utawala wa Bush Ameongeza kusema kingozi huyo wa mrengo wa shoto endapo Bush hatojiuzulu ingekuwa jambo la busara akabiliwe na kura ya maoni ikiwa wamarekani wanamtaka aachie ngazi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com