CARACAS:Chavez atangaza kutaifisha makampuni makubwa nchini Venezuela | Habari za Ulimwengu | DW | 09.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CARACAS:Chavez atangaza kutaifisha makampuni makubwa nchini Venezuela

Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametangaza mipango ya kubinafsisha kampuni za umeme na simu nchini humo ikiwa ni katika hatua kuelekea katika taifa la kisoshalisti.

Chavez akihamasishwa na siasa za kiongozi wa Cuba Fidel Castro amesema kuwa , hatua hiyo ni katika kuelekea kuunda jamuhuri ya kisoshalisti ya Venezuela.

Kiongozi huyo anatarajiwa kuapishwa kesho kwa kipindi cha tatu cha Urais kufuatia ushindi wake mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi uliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com