CANNES : Viongozi wa Afrika wakutana | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CANNES : Viongozi wa Afrika wakutana

Jinsi ya kutumia na kulinda mali asili za Afrika,dhima ya bara hilo duniani na taathira ya ya habari kwa Afrika ni mada kuu katika mkutano wa viongozi wa Afrika ambao umefunguliwa mjini Cannes Ufaransa leo hii.

Mgogoro wa Dafur na Guinea umetia kiwingu mkutano huo wa viongozi 40 wa nchi na serikali wa Afrika.Viongozi wa Sudan,Afrika ya Kati na Chad yumkini wakakutana pembezoni mwa mkutano huo kujadili Dafur.

Zimbabwe imegoma kuhudhuria mkutano huo kwa sababu serikali ya Ufaransa ilisisitiza kwamba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inaweza tu kuhudhuria mkutano huo iwapo itampeleka mtu mwengine badala ya Rais Robert Mugabe.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com