CAMP PENDLETON : Atowa ushahidi wa mauaji ya Muiraq | Habari za Ulimwengu | DW | 07.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAMP PENDLETON : Atowa ushahidi wa mauaji ya Muiraq

Mwanafunzi wa tiba katika jeshi la majini la Marekani amekiri kuhusika katika mauaji ya raia wa Iraq kabla ya kuiambia mahkama jinsi wanamaji wa Marekani walivyotekeleza mauaji hayo ya kikatili na baadae kuficha.

Melson Bacos amekiri kuteka nyara,kula njama na njama ya kutowa taarifa ya uongo baada ya kufikia makubaliano ya kutowa maelezo ya mshtakiwa ambayo yameshuhudia akitowa ushahidi dhidi ya wanamaji saba wanaoshtakiwa kwa mauaji ya Hashim Ibrahim Awad mwenye umri wa miaka 52.

Bacos ameiambia mahkama katika Kambi ya Wanamaji huko Camp Pendleton katika jimbo la Califonia nchini Marekani kwamba alisikia kichefuchefu baada ya Awad kuburuzwa kutoka nyumbani kwake,kupigwa risasi na kuuwawa.

Kifo hicho kilichotokea tarehe 26 April nje ya Baghdad ni mojawapo ya matukio kadhaa ambayo yamechafuwa sifa ya wanajeshi wa Marekani duniani kote.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com