1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon yaweka hai matumaini yake Kombe la Dunia

28 Novemba 2022

Mohammed Salisu ameifungia Ghana bao moja na chipukizi wa Ajax Amsterdam Mohammed Kudus akapachika wavuni magoli mawili na kuipelekea Ghana kupata ushindi muhimu wa 3-2 dhidi ya Korea Kusini katika mechi yao ya kundi H.

https://p.dw.com/p/4KBvS
FIFA Fußball-WM 2022 | Portugal vs. Ghana | Tor GHANA
Picha: Manan Vatsyayana/AFP/Getty Images

 Ghana inakuwa timu ya tatu kutoka Afrika kupata ushindi katika mashindano haya baada ya Senegal na Morocco.

Na Mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar ndiye aliyekuwa nyota katika mechi yao dhidi ya Serbia iliyoishia kwa sare ya mabao matatu ambapo amefunga goli na kumuundia Eric Maxim Choupo Moting bao la kusawazisha.

Kwa matokeo haya ushindani ni mkali mno katika kundi G huku Cameroon sasa ikiwa na pointi moja sawa na Serbia baada ya timu zote kupoteza mechi zao za kwanza.

Fußball WM Katar | Kamerun vs. Serbien | Maxim Choupo-Moting
Eric Maxim Choupo Moting wa Bayern Munich na GhanaPicha: Frank Augstein/AP Photo/picture alliance

Kwengineko Shirikisho la kandanda duniani FIFA limeanzisha uchunguzi baada ya Ujerumani kukiuka sheria zake za mikutano na waandishi wa habari kabla ya ile mechi yao ya jana dhidi ya Uhispania.

FIFA imetangaza Jumatatu kwamba kamati yake ya nidhamu inachunguza sababu iliyopelekea Ujerumani kutowasilisha mchezaji yeyote mbele ya waandishi wa habari siku moja kabla mechi na Uhispania kama sheria za Kombe hilo la Dunia zinavyosema.

Kocha Hansi Flick pekee ndiye aliyehudhuria akitoa sababu kwamba waliwapumzisha wachezaji kwasababu safari ilikuwa ndefu kutoka walikokuwa wachezaji hadi mkutano huo na waandishi wa habari ulipokuwa ukifanyika ndipo walipoamua kuwapumzisha.

Huenda Ujerumani ikaadhibiwa kwa kutozwa faini au kupewa onyo tu.