1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Muslim Brotherhood wakamatwa kabla uchaguzi wa wabunge

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvu

Polisi nchini Misri wamewakamata na kuwazuia wanachama 48 wa Muslim Brotherhood katika msako ikiwa uchaguzi wa wabunge unakaribia. Kwa mujibu wa duru za usalama msako huo uliokuwa mkubwa zaidi ulifanyika katika maeneo ya Giza,Menoufiya na Beni Suef.

Jambo hilo limekosolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu kama Human Rights Watch wanaotoa wito kwa serikali ya Misri kuhalalisha Chama cha Muslim Brotherhood na kuacha kuwakamata.

Kwa mujibu wa serikali Kundi la Muslim Brotherhood halijaidhinishwa kisheria na wafuasi wake hukamatwa kila wakati kwa kufanya mikutano au kuwa na maelezo kulihusu.Kwa upande wao kundi la Muslim Brother ni kundi halali lililo na makao yake mjini Cairo na huwasilisha wagombea wa Urais wa kujitegemea.Kulingana nao siku ya jumatatu kundi hilo lilisajili wagombea 19 kushiriki katika uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Juni 11.Kundi hilo lililinuia kusajili wagombea 20.

Awali raia wa Misri walipuuza uchaguzi wa bunge kubwa la Shoura ila uchaguzi ujao ndio wa kwanza kufanyika baada ya mabadiliko katika katiba yanayolipa bunge hilo madaraka ya kisheria.

Kundi la Muslim Brotherhood lilipata viti 88 katika bunge lililo na nafasi 454 mwaka 2005 lakini halina viti vyovyote kwenye bunge la Shoura.