CAIRO: Mwandishi wa habari ahukumiwa miaka minne jela | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO: Mwandishi wa habari ahukumiwa miaka minne jela

Mahakama ya mjini Alexandria nchini Misri imemhukumu mwandishi mmoja wa habari kifungo cha miaka minne jela kwa kuutukana uislamu na rais wa Misri, Hosni Mubarak, kwenye nakala zake.

Mwandishi wa habari huyo mwenye umri wa miaka 22 hajakanusha kuwa aliandika nakala hizo zilizozikosoa baadhi ya taasisi za kiislamu na rais Mubarak, lakini amehoji ana haki ya kueleza maoni yake.

Mwandishi huyo ni mtu wa kwanza kuhukumiwa nchini Misri kwa kuandika nakala katika mtandao wa mawasiliano wa internet.

Uamuzi wa mahakama ya mjini Alexandria umekosolewa vikali na makundi kadhaa ya kutetea haki za binadamu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com