CAF kuamua kuhusu la Kombe la Mataifa Afrika | Michezo | DW | 11.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

CAF kuamua kuhusu la Kombe la Mataifa Afrika

Shirikisho la Kandanda barani Afrika linatafuta nchi itakayokuwa mwenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani baada ya Morocco kukataa kushikiliakuwa liahirishwe

Hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola imesababisha Morocco kusisitiza msimamo wake kwamba mashindano hiyo ya timu 16, yaliyokuwa yafanyike kuanzia Januari 17 hadi Februari 8 yaahirishwe.

CAF imeziomba nchi nyingine za Afrika kuchukua jukumu hilo kwa dharura lakini hadi sasa haijapata uungwaji mkono. Mkutano wa shirikisho hilo unafanyika mjini Cairo kesho Jumanne na unakabiliwa na uwezekano wa kuahirisha kinyang'anyiro hicho, ila iwapo shirikisho hilo litapata suluhisho haraka.

Morocco inawasi wasi kwamba mashabiki kutoka mataifa ya Afrika magharibi wanaweza kuleta virusi hivyo na kuiweka nchi hiyo katika hatari ya kuhatarisha sekta ya utalii nchini humo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa taifa hilo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afp / dpae / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com