Bw.Steinmeier na Ukanzela . | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.11.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Bw.Steinmeier na Ukanzela .

Waziri wa nje wa Ujerumani Bw.steinmeier akumbana na changamoto kali kutoka kwa Bibi Angela Merkel.

Steinmeier na A.Merkel

Steinmeier na A.Merkel

Juhudi za waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeier,ambae yuko wakati huu ziarani nchini India na anakutana leo na waziri mkuu Monaham Singh,kuwa Kanzela wa Ujerumani baada ya uchaguzi wa mwakani,zimekumbana haraka na matatizo.Ni matatizo yanayobainisha jinsi itakavyokua shida kwake kumtimua bibi Angela Merkel kutoka wadhifa wa kiongozi wa serikali-Kanzela.

Frank Walter Steinmeier,aliteuliwa na chama cha Social Democratic Party (SPD) Septemba mwaka huu, kutoa changamoto kwa Kanzela Angela Merkel katika uchaguzi mkuu wa mwakani nchini Ujerumani.Bw.Steinmeier laki ni anakumbana na shida za kusuluhisha tofauti na mgawiko katika chama chake binafsi na kuwapiku wenzake katika kipindi hiki cha msukosuko wa fedha ulimwenguni.

Katika uchunguzi wa maoni chama cha SPD kiko chini kuliko wakati wowote kabla na unaonesha pia Bw.Steinmeier yuko nyuma sana ya mpinzani wake Bibi Angela Merkel anaeongoza serikali ya muungno unaoyumbayumba na chama cha Bw.Steinmeier (SPD) na chama chake yeye cha Christian democratic party (CDU).

Uchunguzi wa maoni uliochapishwa mwishoni mwa wiki umeonesha 54% ya wajerumani wangemchagua Bibi Merkel kwa kipindi cha pili cha utawala kuwa Kanzela wa Ujerumani akipambanishwa moja kwa moja na Bw.Steinmeier ambae angeondokea 31%.

Bw.Steinmeier mwenye umri wa miaka 52 alijaribu kuzusha mtetemeko wiki iliopita baada ya kukosolewa kwa kukaa kimya katika mzozo wa sasa wa fedha -kimya kilichomfanya kubandikizwa jina la "Kanzela asieonekana".

Hivyo ndivyo magazeti ya Ujerumani yalivyomuita waziri wa nje.

Pale Bibi Merkel alipokua akijiandaa kwa safari ya Washington kuzungumza na viongozi wenzake jinsi gani ya kukifumbua kitandawili cha mzozo wa uchumi na viongozi wa nchi nyengine, alimsangaza kwa kutoa mpango wake wa mambo 9 wa kuutatua mzozo huo Ulaya.

Mpango wa Steinmeier umeitisha ushirikiano miongoni mwa nchi zanachama wa Umoja wa Ulaya ili kukuza nafasi za kazi na nishati inayopatikana tena na tena ili kupambana na msukosuko huo wa fedha .Mpango wake huo lakini ukachochea majadiliano motomoto kuwa ilikuaje kuutangaza mpango huo bila ya kwanza kushauriana na Kanzela Merkel.

Steinmeier alifanya jaribio jengine mwishoni mwa wiki.Muda mfupi tu alipotangaza Bibi Merkel anapanga kukutana na waakilishi wa kampuni la motokaa lililokumbwa na msukosuko OPEL ,nae akatangaza angependa kukutana na waakilishi wa wafanyikazi wa viwanda vya magari tena siku hiyo hiyo.Uamuzi wake wa kukutana nao katika wizara yake ya mambo ya nje ambako desturi hukaribisha wageni kutoka ngambo,kuliwakasirisha wahafidhjina wa CDU.

Hatua hizo za Bw.Steinmeier na jibu zinazopata zimebainisha dhahiri-shahiri shida anazokumbana nazio katika kampeni ya uchaguzi -kipindi ambacho atatumika makamo wa Kanzela na wakati huo huo atataka kuonesha ana msimamo tofauti nae.

Akiwa ni waziri wa nje ,Bw.Steinmeier itampasa ajaribu pia kutota dhana kana kwamba anaingilia uwanja wa waziri wa fedha wa chama chake cha SPD Peer Steinbrueck ambae akishirikiana na Kanzela Merkel,wametunga pamoja mkakati wa kukabiliana na msukosuko wa fedha. Bw.steinbrueck ndie alietunga hasa mpango wa serikali wa kuustawisha uchumi wa dola hili linaloongoza barani ulaya -mpango ambao baadhi ya wanachama wa chama chake SPD wanaona si mkubwa hivyo.

Mzozo wa ndani chamani pia haukumsaidia Bw.Steinmeier.Mabadiliko katika uongozi wa chama hapo septemba yaliopelekea kuondoshwa madarakani kwa Bw.kurt Beck kulishindwa kumaliza mvutano juu ya kushirikiana au kutoshirikiana na chama cha mrengo wa shoto kabisa .

Waziri wa nje Steinmeier na mrithi wa kiti cha uongozi wa chama alichokuwa nacho Bw.Beck-Munterfering,wanapinga kufanya kazi pamoja na chama hicho cha mrengo wa shoto kabisa.Hatahivyo, wsalishindwa kumzuwia Bibi Andrea Ypsiklanti huko Frankfurt ,mkoani Hesse katika jaribio lake la kuchaguliwa waziri mkuu wa mkoa huo kwa msaada wa chama hicho cha mrengo wa shoto-Link Partei.Jaribio la Bibi Ypsilanti lilitiwa munda na akashindwa hatahivyo, hii haikuzuwia kutertemsha umaarufu wa chama cha SPD hadi kima cha 23%.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com