BUYERN NA WOLFSBURG ZATINGA NUSUFAINALI | Michezo | DW | 28.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

BUYERN NA WOLFSBURG ZATINGA NUSUFAINALI

Hapo jana huko Munich nchini Ujerumani kulikuwa narobofainali ya kombe la Ujerumani la kabumbukati ya mafahari wa mji huo, Buyern Munich na Munich 1860.

default

Kocha wa Bayern Munich Ottmar Hitzfeld

Mbali ya pambano hilo pia kulikuwa na robofainali nyingine kati ya Wolfsburg na Hamburg.


Buyern Munich na Wolfsburg jana usiku walifanikiwa kutinga nusufainali ya kombe la Ujerumani baada ya kushinda memchi zao dhidi ya Munich 1860 na Hamburg.Mechi zote mbili zilihushuhudia muda ukirefushwa kumpata mshindi.


Buyern Munich iliwabidi kufanya kazi ya ziada kuwashinda vijana wenzao wa Munich ambao hujulikana kama simba wa Munich Munich 1860.


Munich ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Frank Riberry kwa mkwaju wa penalti katika muda wa nyongeza baada ya kuwa sare katika dakika tisini za kawaida.


Penalti hiyo ambayo ilionekana ya utata ilitokana na mshambuliaji wa Buyern Munich Miroslav kuangushwa ndani ya 18, lakini picha za televisheni zilionesha kuwa alikuwa nje ya box.Franky Ribbery hakufanya kosa kuukwamisha mpira wavuni na kufuzu kwa nusufainali.


Kocha wa Buyern Munich Ottmar Hitzfeld alikiri ya kwamba mechi ilikuwa ngumu.


Mapema katika robofainali nyingine Hamburg ililambishwa mchanga na Wolfsburg kwa kuchapwa mabao 2-1.


Kiungo wa Hamburg Van de Vaar mara baada ya kutimuliwa na wenzao hao wa bundesliga alisema


Buyern Munich na Wolfsburg zinaunagana na timu ya daraja la pili Carl Zeiss Jena na Borrussia Dormund zilizofuzu hapo juzi katika robofainali nyingine.


Katika masumbwi mbabe wazamani wa msumbiwi duniani, Evandr Holyfield ametanabaisha kuwa yuko katika mazungumzoi na mbabe mwengine wa zamani Mike Tyson kupanda tena ulingoni.


Akinukuliwa mjini London Holyfield alisema kuwa meneja wa Tyson alimpigia simu akiwambia kuwa Tyson anataka kurudiana naye tena ulingoni kufuatia pambano lao la mwaka 1997.


Katika pambano hilo ambalo lilikuwa la pili kati ya majogoo hao wa masumbwi, Tyson ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 42 alimg´ata sikio Holyfield mwenye umri hivi sasa wa miaka 45 na kutema kipande cha sikio sakafuni.►◄

 • Tarehe 28.02.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DFN3
 • Tarehe 28.02.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DFN3
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com