1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush kuizuru Russia wiki ijayo.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVeg

Washington.

Rais wa Marekani George W. Bush amesema kuwa atafanya ziara nchini Russia wiki ijayo ili kujadili suala la uwekaji wa kituo cha makombora ya kujihami na rais anayeondoka madarakani Vladimir Putin.

Russia imeikosoa sana mpango huo wa Marekani wa ulinzi wa makombora, ambapo kituo cha kukinga makombora hayo kitajengwa nchini Poland na mfumo wa rada utakaokuwa nchini jamhuri ya Chek. Marekani imesema kuwa mfumo huo unahitajika kupambana na uwezekano wa kitisho kutoka Iran, lakini Russia inahofu kuwa unaweza kutumika dhidi ya Russia pia.