1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush atoa mwito kwa Misri

16 Januari 2008

Rais Bush wa Marekani akikamilisha ziara yake ya Mashariki ya kati huko Sharm el Sheik aitaka Misri kuendeleza demokrasi.

https://p.dw.com/p/Cqxf
Bush Sharm el SheikhPicha: AP Photo

Rais George Bush wa marekani akikamilisha leo ziara yake ya siku 8 katika Mashariki ya kati alitaka Misri huko Sharm el Sheikh –kituo chake cha mwisho cha ziara hii, kushika usukani katika kuendeleza mbele na kuimarisha demokrasia katika Mashariki ya Kati.

Rais Bush pia alizitaka Syria na Iran kukomesha kujiingiza katika mambo ya ndani ya Lebanon na kuzitaka nchi za eneo hilo kumuungamkono waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora.

Rais Bush alimuambia mwenyeji wake rais Hosni Mubarak wa Misri na ninamnuklulu,

„Umepiga hatua kufungua milango ya uchumi na mageuzi ya kidemokrasia.“ …….“ Matarajio yangu sasa ni kuwa serikali ya Misri itajenga zaidi juu ya matufali hayo muhimu na kuwapa wananchi wa taifa hili la kujivunia sauti zaidi katika mustakbala wao.“-Bush alimwsambia Hosni Mubarak mbele ya maripota huko Sharm el Sheikh adhuhuri ya leo.

Marekani karibuni hivi imekuwa ikiikosoa Misri na kuonesha wasi wasi katika rekodi ya Misri ya haki za binadamu na kaama ishara ya kupooza kwa usuhuba kati ya Washington na Cairo,Bush alipitisha masaa 3 nchini Misri.

Mwaka jana Marekani ilikariri mwito wake wa kudai kuachwa huru kwa mpinzani wa Misri Ayman Nur-dai ambalo lilizusha hasira katika serikali ya cairo ikidai Marekani inaingilia mambo yake ya ndani.

Bush akamuambia Mubarak na ninamnukulu,

„Kutokana na mchango mkubwa unaotoa,naamini kwa dhati kuwa Misri inaweeza kuchangia mno katika kuleta uhuru na haki na kwamba ulimwengu unaikodolea macho Misri.

Uhusiano na Misri pia umezorota juu ya ila za Marekani kuwa Misri haiulindi mpaka wake barabara na mwambao wa Gaza inayotawaliwa sasa na chama cha Hamas na kwamba eti silaha zinapita kuingia huko. Kuhusu juhudi zake za kufumbua kitandawili kati ya wapalestina na waisrael-mojawapo ya ajenda ya ziara yake hii ya nchi 8 za Mashariki ya kati,

Rais Bush alielezea matumaini juu ya kufanikiwa kwa juhudi alizozianzisha kwa sababu anasema,

„naamini uongozi nchini Israel na hata ule wa wapalestina umejitolea kuungamkono.Na najua mataifa ya jirani nayo ni tayari pia kuungamkono.“

Akielekea mzozo nchini Lebanon, rais Bush alizitaka syria na Iran kuacha kutia mkono wao katika maswali ya Lebanon na akazitaka nchi za eneo hilo kumuungamkono waziri mkuu Fouad Siniora.

Lebanon imeahirisha uchaguzi war ais kwa mara ya 12 wiki iliopita licha ya juhudi zilizofanywa na Arab League-jumuiya ya nchi za kiarabu –jambo ambalo limeiacha Lebanon bila rais kwa mara ya kwanza tangu vita vya kienyeji vya 1975-90.