Bush aendeleza ziara yake mashariki ya kati | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 11.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Bush aendeleza ziara yake mashariki ya kati

---

RAMALLAH

Rais George Bush wa Marekani anaendelea na ziara yake mashariki ya kati leo hii akielekea Katika juhudi za kuzitia moyo nchi za kiarabu kuungana nae katika kufanikisha mpango wa amani kati ya Israel na Palestina.Katika siku ya pili ya ziara yake hapo jana rais Bush alitumia matamshi makali kuelekea taifa la kiyahudi la Israel akilitolea mwito taifa hilo kuondoka katika ardhi ya wapalestina Ukingo wa magharibi waliyoinyakua miongo minne iliyopita.

Kwa upande mwingine rais Huyo wa Marekani anayewania kujitakasa jina katika mashariki ya kabla ya kuondoka madarakani mwaka ujao,amewataka wapelstina kukabiliana na wanamgambo akisema mpango wa amani na Israel lazima uhakikishe taifa hilo linapata usalama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com