1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUR HAKABA: Mji wa Bur Hakaba watekwa na majeshi ya Somalia

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0Q

Wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia, wameuteka mji wa Bur Hakaba baada ya mapigano makali kati yao na wanamgambo wa kiislamu.

Kwa mujibu wa wakaazi wa mji huo na makamanda wa jeshi, wanajeshi waliokuwa wamejihami na silaha nzito waliuvamia mji wa Bur Hakaba, yapata kilomita 60 kusini mashariki mwa Baidoa, makao makuu ya serikali ya mpito ya Somalia.

Duru zinasema uvamizi huo ulizusha mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wanaounga mkono vuguvugu la mahakama za kiislamu la Al Bayan. Wanamgambo hao walilazimika kuutoroka mji huo.

Naibu kiongozi wa usalama wa mahakama za kiislamu, Sheikh Muhktar Robow, amethibitisha kutekwa kwa mji wa Bur Hakaba na majeshi wa Somalia na Ethiopia.