Bundesliga.Dortmund bingwa wa nusu msimu | Michezo | DW | 05.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga.Dortmund bingwa wa nusu msimu

Katika ligi ya soka ya Ujerumani Bundesliga, Schalke 04 imeigaragaza Bayern Munich kwa mabao 2-0.

default

Bastian Schweinsteiger wa Bayern Munich (kushoto) akipambana na Christoph Metzelder wa Schalke

Borussia Möenchengladbach wameangukia pua baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Hannover.

Eintracht Frankfurt nayo ikaibuka mshindi dhidi ya Mainz kwa kuifunga mabao 2-1.

Katika mechi nyingine Freiburg iliishinda Sport Verein Hamburg bao 1-0, wakati Vfb Stuttgart na Hoffenheim zilitoshana nguvu pale zilipotoka suluhu ya bao 1-1 nazo Wolfsburg na Werder Bremen hakupatikana mbabe baada ya timu hizo kutoka sare bila kufungana.

Borussia Dortmund ambayo inamiadi leo Jumapili na 1FC Nuremberg imejipatia taji lisilo rasmi la ubingwa wa majira ya mapukutiko, kwa mara ya tatu katika historia ya club hiyo. Hadi sasa Borussia Dortmund imeshinda michezo 12 kati ya 14 msimu huu.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Sekione Kitojo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com