1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vilabu vya Bundesliga vyaimarisha usalama wao

Admin.WagnerD20 Novemba 2015

Michuano ya ligi kuu ya kandanda Ujerumani – Bundesliga inarejea hii leo, tangu kutokea mashambulizi ya kigaidi mjini Paris, na vilabu vimewahakikishia mashabiki kuwa usalama wao utazingatiwa

https://p.dw.com/p/1H9iG
Bundesliga Werder Bremen vs 1. Hamburger SV
Picha: imago/nph

Mashabiki pia wametakiwa kutowasha fataki wakati wa michuano kwa sababu inaweza kusababisha hofu ya kutokea mkanyagano wa watu.

Kurejea kwa kandanda la ligi ya nyumbani baada ya kipindi cha mapumziko kwa ajili michezo ya kimataifa huwa kunasubiriwa kwa hamu lakini tunatarajia kuona mazingira ya kipekee katika viwanja vya Bundesliga wikendi hii baada ya mashambulizi ya Paris.

Viongozi wa ligi Bayern Munich watapambana na Schalke hii leo katika mpambano ambao unatarajiwa kuwa na ulinzi ulioimarishwa.

Nambari tatu Wolfsburg watalenga kuendeleza kampeni ya kujiimarisha katika nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya wakati watawaalika Werder Bremen. Hertha Berlin inayoshikilia nafasi ya nne, itapambana na Hoffenheim kesho Jumapili.

Katika kivumbi cha kuepuka kushushwa ngazi, Stuttgart ambao wako katika nafasi ya 16 wanawaalika washika mkia Augsburg. Borussia Moenchengladbach watakuwa na miadi na Hanover, wakati Eintracht Frankfurt wakipambana na Bayer Leverkusen nao Cologne wakiangushana na Mainz.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP
Mhariri: Yusuf Saumu