Bundesliga yarejea uwanjani | Michezo | DW | 20.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bundesliga yarejea uwanjani

Ligi ya Bundesliga inarejea uwanjani,huku mashabiki wakielekeza macho na masikio yao katika mchezo wa watani wa jadi ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya mabingwa watetezi Dortmund na mahasimu wao wa jadi Schalke.

allgemein, Feature, Randmotiv, die Polizei zwischen den beiden Fanlagern, Polizist, Polizisten, Sicherheit, Ueberwachung, Überwachung, Security, Ordner, Fussball 1. Bundesliga, Spieltag 31, FC Schalke 04 (GE) - Borussia Dortmund (DO) 1:2, am 14.04.2012 in Gelsenkirchen / Deutschland

Mashabiki wa Dortmund na Schalke katika pambano la watani wa jadi

Bayern Munich itakuwa wageni wa Fortuna Dusseldorf, wakitaraji kuvunja rekodi ya Bundesliga ya kushinda mchezo wake wa nane mfululizo katika michezo minane ya mwanzo wa ligi.

Bayern Munich's Brazilian defender Dante reacts during the German first division Bundesliga football match FC Schalke 04 vs FC Bayern Munich on September 22, 2012 in Gelsenkirchen, western Germany. Bayern Munich won the match 0-2. AFP PHOTO / PATRIK STOLLARZ RESTRICTIONS / EMBARGO - DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER MATCH. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050. (Photo credit should read PATRIK STOLLARZ/AFP/GettyImages)

Mchezaji wa Bayern Munich Dante

Mashabiki wa soka nchini Ujerumani wanasubiri kwa hamu mchezo wa nane wa ligi ya Ujerumani Bundesliga ambapo leo (20.10.2012) timu zitaingia viwanjani kuwania points tatu muhimu.

Mapumziko ya wiki mbili ambapo timu ya taifa ilikuwa na heka heka za kuwania tikiti ya kucheza katika fainali za kombe la dunia, yalikuwa marefu mno, wakati mashabiki wakisubiri kwa hamu mpambano wa kukata na shoka wa mahasimu wakubwa katika Bundesliga. Borussia Dortmund inawakaribisha mahasimu wao wakubwa , na watani wa jadi Schalke 04.

Linapofanyika pambano la watani hawa wa jadi Ujerumani yote hukodolea macho mpambano huu na kusahau kuwa kuna timu nyingine zinashindana katika Bundesliga. Hii ni mama wa "Derby ", zote.

Mfano wake naweza kuulinganisha na pambano kati ya Yanga na Simba mjini Dar Es Salaam.

Dortmund imekwisha nyakua points kumi kutoka points 12 katika mapambano 4 ya watani hawa wa jadi , lakini imeshinda mapambano mawili tu kati ya 13 yaliyopita nyumbani dhidi ya mahasimu wao hao.

Pamoja na hayo kila kitu kinawezekana katika mchezo wa watani wa jadi , amesema hivyo mlinzi wa Schalke 04 Benedict Höwedes. Huu unakuwa mchezo tofauti kabisa, ulio na hamasa tofauti kabisa. Mashabiki huishangiria timu yao kwa nguvu zote, na timu zote hujaribu kwa njia zote.

Höwedes ana matumaini kuwa Dortmund itaziachia points mara hii.

Bayern ina kibarua kigumu

Bayern Munich inatarajia kuweka rekodi ya kushinda mara nane mfululizo mwanzoni mwa msimu, wakati ikiwa ugenini nyumbani kwa Fortuna Dusselsdorf.

Hata hivyo huo hautakuwa mchezo rahisi kwa timu hiyo ambayo imenyakua ubingwa wa ligi ya Ujerumani mara nyingi zaidi.

Kwa kawaida Dusseldorf haikubali kufungwa nyumbani misimu yote, na mara nyingi imefanikiwa kupata sare, na msimu huu wa 2012 , haijafungwa nyumbani hadi sasa.

Jorome Boateng mlinzi wa Bayern Munich amekiri hata hivyo kuwa huo utakuwa mchezo mgumu sana kwao.

Dhidi ya Hannover 96 , timu inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi Eintracht Frankfurt inataka kuimarisha nafasi yake baada ya kurejea katika ligi daraja la kwanza msimu huu.

Timu hiyo hadi sasa haijashindwa ikicheza nyumbani na hupata katika kila mchezo takriban mabao mawili. Hadi sasa imeshinda mara tano katika michezo saba iliyocheza, na ndio sababu kocha wa Hannover 96 Mirko Slomka amekionya kikosi chake kinachoingia uwanjani leo na Eintracht Frankfurt.

Bayer Leverkusen inawasubiri nyumbani Mainz 05, na kocha wa Leverkusen amewaonya wachezaji wake kutoidharau Mainz.

Maji ya shingo

Maji yako shingoni mwa kocha Felix Magath wa Wolfsburg. Wolfsburg iko mkiani mwa msimamo wa ligi na iko maili kadha mbali na lengo lake ililojiwekea msimu huu. Pambano lake dhidi ya Freiburg leo litaamua hatima ya kocha huyo.

Fussball 1. Bundesliga 2. Spieltag VfL Wolfsburg - Hannover 96 am 02.09.2012 in der Volkswagen Arena in Wolfsburg Felix Magath ( Trainer Wolfsburg ) Foto: Revierfoto

Kocha wa VfL Wolfsburg Felix Magath

Werder Bremen itajitupa uwanjani jioni ya leo kupambana na Borussia Moenchengladbach. Jumapili FC Nürnberg itakwaana na FC Augsburg, na pia Hambug SV itakuwa na kibarua dhidi ya VFB Stuttgart.

Katika Premier League, mshambuliaji Nani wa Manchester United amekiri kuwa kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson kitakuwa na kibarua kigumu kuishinda Stoke City.

Soccer - Barclays Premier League - Manchester United v Newcastle United - Old Trafford.Luis Nani, Manchester United URN:9324567

Luis Nani mchezaji wa Manchester United

Pamoja na hayo kutakuwa na mpambano mwingine kati ya Tottenham Hotspurs ikiikaribisha Chelsea, Liverpool ikiwa nyumbani kupimana nguvu na Reading, wakati mabingwa watetezi Manchester City wanapimana ubavu na West Bromwich Albion. Arsenal inajaribu bahati yake nyumbani kwa Norwich City.

Jumapili ni zamu ya Sunderland na Newcastle kuonyesha kazi, na Queens Park Rangers ina miadi na Everton.

Real Madrid imekumbwa na janga la majeruhi kikosini katika kile magazeti ya Uhispania ilichokiita virusi vya FIFA, baada ya mapumziko ya michuano ya timu za taifa.

Real Madrid itawakosa wachezaji Alvaro Arbeola , Fabio Coentrao na mlinzi wa kushoto Marcelo ambaye anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuvunjika mguu katika mazowezi akiwa na timu ya taifa ya Brazil.

Real Madrid's coach Jose Mourinho gestures during their Spanish King's Cup quarter-final first leg El Clasico soccer match against Barcelona at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, January 18, 2012. REUTERS/Felix Ordonez (SPAIN - Tags: SPORT SOCCER)

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho

Real inakwaana na Celta Vigo, wakati Barcelona iko ugenini dhidi ya Deportivo la Coruna. Valencia ina miadi na Athletico Bilbao na Real Sociedad inapambana na Atletico Madrid.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman