1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga ya wanawake kuendelea tena Mei 29

21 Mei 2020

Chama cha Soka Ujerumani DFB kimesema Ligi Kuu ya Ujerumani kwa wanawake itaanza tena kufuatia kusitishwa kwake Mei 29 kutokana na virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3caLl
Fussball DFB Pokal Finale  Frauen l VFL Wolfsburg vs Freiburg l Jubel 1:0
Picha: Imago/regios24/D. Simka

DFB imesema ligi hiyo ni mojawapo ya michezo iliyokuwa imepewa ruhusa ya kuendelea na mamlaka za afya Ujerumani. Mamlaka hizo ndizo zilizo na usemi wa mwisho kuhusiana na kutoa idhini ya kuendelea kwa michezo Ujerumani.

"Nina furaha sana kwamba vilabu vya Bundesliga ya wanawake vimeonyesha umoja kuhusiana na kuendelea kwa msimu," alisema rais wa DFB Fritz Keller.

Bundesliga ya wanaume ilianza tena kucheza mechi zake Jumamosi tarehe 16 Mei, hiyo ikiwa ni ligi ya kwanza kuu ya Ulaya kurudi uwanjani.