1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga kutifua vumbi

Grace Kabogo
18 Septemba 2020

Bayern Munich inaanza leo kusaka taji lake la tisa la Bundesliga, itakapoteremka uwanjani Allianz Arena mjini Munich kuikabili Schalke 04.

https://p.dw.com/p/3iglK

Je nini kitarajiwe katika mchezo wa leo dhidi ya mabingwa waliotoroka na mataji matatu msimu huu? Kuna mjadala mkubwa katika Ligi Kuu ya Kandanda Ujerumani, Bundesliga iwapo kuna timu inaweza kuwavua ubingwa Bayern, washukiwa wa kawaida wametajwa, wakiongozwa na Borussia Dortmund. Kuhusu mchezo wa leo pamoja na ubabe wa Bayern katika Bundesliga Sudi Mnette amezungumza na Sekione Kitojo wa dawati la michezo.