BUKHARA : Steinmeir aendelea na ziara Asia ya Kati | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BUKHARA : Steinmeir aendelea na ziara Asia ya Kati

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amewasili nchini Uzbekistan katika kituo cha pili cha ziara yake ya mataifa matano ya Asia ya Kati.

Waziri huyo wa Ujerumani amekuwa na mazungumzo na Rais Islam Karomov wa Uzbekistan juu ya masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na haki za binaadamu na kudokeza kwamba Umoja wa Ulaya unaweza kuiondolea nchi hiyo baadhi ya vikwazo vyake ikiwa jimbo hilo la zamani la Muungano wa Urusi litachukua hatua zaidi kuendeleza maadili ya demokrasia.

Makundi ya haki za binaadamu yamesema polisi iliwapiga risasi na kuwauwa takriban waandamanaji 700 katika mji wa Andizhan mwezi wa Mei uliopita.

Wito wa Umoja wa Ulaya kutaka iundwe tume huru kuchunguza mauaji hayo hadi sasa umekuwa ukikatiliwa na uongozi wa serikali ya Uzbekistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com