1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA : Wabunge wamtimuwa Spika

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIM

Wabunge wa Burundi hapo jana wamepiga kura kumtimuwa spika wa bunge Immaculee Nahayo ambaye alikuwa akionekana kuwa yu karibu mno na kiongozi wa zamani wa chama tawala nchini humo.

Hussein Rajabu kiongozi mwenye ushawishi wa chama tawala cha CNND- FDD ametimuliwa katika uongozi mwezi uliopita na tokea wakati huo washirika wake kadhaa wamekuwa wakitimuliwa madarakani.

Nahayo ameondolewa hapo jana kwa azimio linalomshutumu kuvunja sheria za bunge na kuleta machafuko.

Wabunge 86 kati ya 118 walipiga kura kuunga mkono kutimuliwa kwa spika huyo ambaye ameapa kupinga uamuzi huo mahkamani.Amesema amesikitishwa kuona watu wanaotakiwa kulinda sheria wamekuwa wa kwanza kuikiuka.

Rajabu mwenyewe ameulezea uamuzi huo kuwa ni mapinduzi na utasababisha kukosekana kwa utulivu nchini humo.

Kabla ya kuanguka kwake Rajabu inasemekana kuwa alikuwa na ushawishi mkubwa kabisa nchini Burundi kwa kuwa na udhibiti wa fedha na vitengo vya ujasusi vya chama cha CNDD-FDD.