BUJUMBURA : Mkamo wa kwanza wa rais ajiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BUJUMBURA : Mkamo wa kwanza wa rais ajiuzulu

Makamo wa kwanza wa rais wa Burundi Martin Nduwimana ambaye chama chake cha zamani cha UPRONA ni miongoni mwa makundi ya upinzani yanayosusia bunge kujaribu kulazimisha mabadiliko ya baraza la mawaziri amejiuzulu hapo jana usiku.

Nduwimana ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba anataka kuleta suluhisho kwa mzozo wa muda mrefu uliodhoofiosha taasisi za nchi hiyo.

Amesema ameamuwa kujiuzulu baada ya mazungunmzo yake na wenzake wa zamani ambao walimn’gowa kutoka UPROMA hapo mwezi wa Augusti baadhi yao wakimwita kuwa haini kwa kushirikiana na serikali.

UPRONA na chama kengine cha upinzani cha FRODEBU vitanaka baraza zima la mawaziri la serikali ya Burundi libadilishwe kutokana na shutuma za ukiukaji wa haki za binaadamu na kushindwa kukomesha rushwa nchini humo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com