1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUDAPEST:Mamia wafa barani ulaya kutokana na joto kali

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfZ

Mamia ya watu wamekufa kutokana na joto kali lililoikumba Ulaya, ambapo nchini Hungary zaidi ya watu 500 wamekufa kutokana na joto.

Kiwango cha joto katika eneo la kusini mashariki mwa Ulaya kimefikia nyuzi joto 45, huku Romania, Ugiriki na Bulgaria zikiathiriwa zaidi.

Halikadhalika hali hiyo imesababisha majanga ya moto katika nchi za Italia, Macedonia na maeneo ya pwani ya Croatia na Serbia.

Nchini Uingereza eneo kubwa la katikati na magharibi mwa nchi hiyo bado liko katika maji kutokana na mafuriko makubwa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.

Mamia ya familia wameendelea kukosa huduma ya maji safi na umeme, kutokana na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Wataalam wa hali ya hewa wanasema kuwa hali ya joto na mafuriko yametokana na mabadiliko ya hali hewa duniani.