BUDAPEST: Hangary yaadhimisha mwaka wa 50 tokea kuanguka utawala wa kikoministi | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BUDAPEST: Hangary yaadhimisha mwaka wa 50 tokea kuanguka utawala wa kikoministi

Sherehe zinafanyika nchini Hungary kuadhimisha mwaka wa 50 tokea kuanguka kwa utawala wa kikoministi japokuwa migawanyiko bado ipo na kusababisha upinzani kususia shughuli rasmi. Polisi nchini Hungary wametawanya waandamanaji nje ya jebgo la bunge licha ya hakikisho iliokuwa imetolewa kwamba waandamanaji wataruhusiwa kubaki katika sehemu hiyo. Sherehe za kwanza zilianza jana jumapili katika jengo la serikali la bustani na kuhudhuriwa na rais wa Ujerumani Horst Kohler. Wajumbe kutoka nchi 50 wanashiriki katika sherehe nje ya bunge na watayatembelea makaburi ya Imre Nagy, aliyekuwa waziri mkuu wakati wa mapinduzi mwaka wa 1956 na mmoja kati ya watu kiasi ya 200 wengine, waliouawa kwa ksuhiriki katika uasi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com