BUCHAREST:Köhler aitaka Romania kuondoa rushwa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BUCHAREST:Köhler aitaka Romania kuondoa rushwa

Rais wa Ujerumani Horst Köhler ameitaka serikali ya Romania kuongeza zaidi mapambano dhidi ya rushwa.

Rais Köhler alisema hayo baada ya mkutano na mwenyeji wake Rais Traian Basescu wa Romania mjini Bucharest.

Rais huyo wa Ujerumani yuko katika ziara ya mataifa matatu ya Balkan, ambapo mbali ya Romania atatembelea pia Bulgaria na Bosnia-Herzegovina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com