BRUSSELS:Majeshi ya amani kupelekewa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS:Majeshi ya amani kupelekewa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Ulaya huenda ukapeleka majeshi ya kulinda amani katika nchi za Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati ili kuwalinda raia wanaoathirika na ghasia kwenye eneo jirani la Darfur lililoko nchini Sudan.Maafisa wa Umoja huo wanakutana jumatatu ijayo kujadilia pendekezo hilo baada ya Umoja wa Mataifa kutoa ombi la msaada.Pendekezo hilo huenda likaidhinishwa mwanzoni mwa mwezi Septemba na majeshi kupelekwa ifikapo mwezi Oktoba.Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na takriban majeshi alfu 1 hadi 2500 na kuhusisha zaidi taifa la Ufaransa.

Shirika la Kutetea haki za binadamu Human Rights watch kwa upande wake linaonya kuhusu mchanganyiko ambao huenda ukatokea kati ya kikosi cha Ufaransa au Umoja wa Ulaya kwani Ufaransa inahusiana kwa karibu na mataifa yote mawili.

Mwezi jana Sudan ilikubali kupelekwa kwa majeshi ya shirika ya Umoja wa mataifa na Afrika ili kulinda amani katika eneo la Darfur.Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na majeshi takriban alfu 20.Nchi za Sudan na Chad zinalaumiana kwa kuunga mkono vitendo vya uasi katika nchi zote mbili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com