1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS.Iran kuwekewa vikwazo vya umoja wa mataifa

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSk

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa umoja wa ulaya wameamua kuutekeleza mpango wa umoja wa mataifa juu ya kuiwekea Iran Vikwazo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa liliamuru vikwazo kwa Iran mwishoni mwa mwaka jana baada ya Tehran kukataa kusimamisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier amesema kuwa Iran sasa imeonyesha hamu ya kutaka kurudi katika meza ya mazungumzo juu ya mpango wake wa nyuklia, lakini umoja wa ulaya utasubiri hadi pale Iran itakapo toa ombi rasmi la kutaka mazungumzo hayo yafufuliwe. Waziri Steinmier alikutana na mpatanishi mkuu wa maswala ya nyuklia wa Iran katika mkutano wa kimataifa wa usalama uliomalizika mjini Munich mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wakati huo huo mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Marti Ahtisaari amewasilisha pendekezo lake kuhusu hali ya baadae ya Kosovo kwa mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa ulaya.

Mpango wake unapendekeza kuwepo uhuru wa kadiri kwa jimbo la Serbia ambalo liko chini ya umoja wa mataifa tangu mwaka 1999.

Serikali ya Belgrade hata hivyo imekataa rasimu ya mpango huo wa Ahtisaari kwa kusemna kuwa italigawa taifa la Serbia.