BRUSSELS: Umoja wa Ulaya watoa mswada wa nishati | Habari za Ulimwengu | DW | 09.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya watoa mswada wa nishati

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels, Ubelgiji, wamefikia mswada wa makubaliano ya pamoja kuhusu matumizi ya nishati.

Makubaliano hayo yanaweka kiwango cha asilimia 20 cha matumizi ya nishati mbadala katika mataifa ya Umoja wa Ulaya kufikia mwaka wa 2020 katika mkakati wa kupambambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mswada huo uliowasilishwa na Ujerumani, mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya, unatoa mapendekezo vipi wanachama 27 wa umoja huo wanavyochangia kulifikia lengo la Ulaya la kutumia nishati mbadala kama vile nishati inayotokana na jua, upepo na umeme kutokana na maji.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anataka kuwepo mazungumzo zaidi kwa kuwa ufanisi bado haujapatikana.

´ Hatujafanikiwa bado. Hilo ninataka kulieleza wazi kwa sababu hapa jioni ya leo tumekuwa na mazungumzo mbalimbali. Bado kuna haja ya kufanya mazungumzo zaidi kulishuhgulikia swala hili. Kuna mazungumzo mazuri kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa hivi kwamba sijaachwa bila matumaini.´

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ana matumaini ya kufikiwa mkataba wa mkakati wa muda mrefu utakaojumulisha swala la nishati na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuibinya Marekani na mataifa mengine yaliyoendelea kiviwanda na mataifa yanayoinukia kiuchumi yaige mfano wa Umoja wa Ulaya katika kupamabana na ogezeko la ujoto duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com