1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya kuongeza misaada Kongo.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmJ

Tume ya umoja wa Ulaya imependekeza kuongeza mara dufu msaada wa maendeleo ya umoja huo kwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , ili kusaidia ujenzi mpya nchini humo kufuatia uchaguzi wa hivi karibuni.

Tume hiyo imekuwa mfadhili mkuu, ikitoa fedha kwa ajili ya hatua za uchaguzi nchini Kongo tangu 2001, ikitoa kiasi cha Euro milioni 165 katika kiasi karibu Euro milioni 400 katika gharama zote za uchaguzi.

Mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya wanapaswa hata hivyo kulikubali pendekezo hilo. DRC ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia katika muda wa miaka 40 mwezi uliopita, na rais Joseph kabila Kabange amedhibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo wiki iliyopita.