1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Majadiliano kuanzishwa upya na Serbia

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtt

Umoja wa Ulaya umearifu kuwa siku ya Jumatano yataanzishwa tena majadiliano ya kuwa na uhusiano wa karibu na Serbia.Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Baroso amehalalisha uamuzi huo. Amesema,serikali ya Belgrade,sasa inashirikiana na Mahakama ya Uhalifu wa Vita ya Umoja wa Mataifa mjini The Hagaue.Majadiliano hayo yalisitishwa mwaka jana kwa sababu Belgrade haikutimiza ahadi ya kumkamata mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya halaiki,Ratko Mladic.Lakini juma lililopita,Serbia ilimfikisha mahakamani mjini The Hague,jemadari wa zamani,Zdravko Tolimir baada ya kumkamata mashariki ya Bosnia.Jemadari huyo wa zamani alie Mserb wa Bosnia,alikuwa akisakwa kwa mashtaka ya mauaji ya halaiki.