1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brexit,Greenland na Mgogoro wa Italia Magazetini

Oumilkheir Hamidou
22 Agosti 2019

Kiu cha Uingereza za kujitoa kwa kila hali katika Umoja wa Ulaya, mgogoro wa kisiasa nchini Italia na wazo la rais wa Marekani Donald Trump la kutaka kukinunua kisiwa cha Greenland kinachomilikiwa na Denmark magazetini.

https://p.dw.com/p/3OJXf
London Demonstrant als Boris-Johnson-Clown verkleidet
Picha: AFP/D. Leal-Olivas

Tunaanzia katika ujia wa maji unaoitenganisha Uingereza na bara la Ulaya. Waziri mkuu wa nchi hiyo ya kifalme, Boris Johnson amefika ziarani  barani Ulaya; Ametuwa kwanza mjini Berlin na baadae leo anakaribishwa Paris, lengo likiwa  kujaribu kutetea azma yake ya kuitoa Uingereza kwa vyovyote vile October 31 itakapowadia. Mhariri wa gazeti la "Hessische Niedersächsische Allgemeine" anashuku kama atafanikiwa. Gazeti linaandika:"Boris Johnson hajali athari za kiuchumi zinazoashiriwa na wataalam kadhaa mashuhuri. Bendera yake; "Kwanza Brexit" ameshaifikisha Berlin na Paris akitaraji kwa kutishia kuitoa kwa vyovyote vile nchi yake katika Umoja wa ulaya October 31 itakapofika, ataweza kuwatanabahisha kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ili utaratibu wa kujitoa nchi yake katika Umoja wa ulaya-Brexit ujadiliwe upya. Amechelewa. Merkel na Macron hawaiungi mkono kabisa fikra hiyo. Kwasababu kifungu cha Backstop, yaani hakikisho kwamba mpaka kati ya  jamhuri ya Ireland na jimbo la Ireland hautafungwa, hakitoguswa-kwasababu kifungu hicho ni muhimu katika kudhamini usalama katika kisiwa hicho. Ujumbe wa Umoja wa ulaya kwa hivyo kwa Ireland ni huu "Kamwe hatutokuacha peke yako.."

Trump amezea mate kisiwa cha Greenland

 Risala za rais wa Marekani kupitia mtandao wa Twitter hazikuanza leo. Lakini ya safari hii imepindukia mipaka. Anamshinikiza mshirika wa Marekani katika jumuia ya kujihami ya NATO amuuzie sehemu ya ardhi yake: Kisiwa cha  bahari ya  Arctic katika ncha ya kaskazini ya dunia yetu  cha Greenland". Gazeti la "Mannheimer Morgen" linahisi hakuna haja ya watu kushangaa. Gazeti linaendelea kuandika: "Inakadiriwa kwamba chini ya mlima wa theluji wa mita 3400 unaofunika sehemu kubwa ya kisiwa hicho, kuna madini mengi yenye thamani. Kila theluji hiyo inapoyayuka haraka haraka ndio vizuri zaidi kwa rais huyo mfanyabiashara ambae wakati huo ataachilia mbali mipango ya kwenda kwenye sayari ya Mars na badala yake atapanua maeneo ya kuyatawalia kikoloni."

Salvini ajichimbia kaburi kisiasa

 Mada yetu ya mwisho inatufikisha Italia ambako mgogoro wa kisiasa unatokota tangu aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Metteo Salvini alipotoa wito wa kuitishwa uchaguzi kabla ya wakati. Gazeti la "Freie Presse" linaandika:"Kwa mara nyengine tena Salvini analenga kitu kimoja tu: Anajilenga yeye mwenyewe. Vurugu za kisiasa hakuzitilia maanani. Lakini kiongozi huyo wa chama cha Liga ameula na chuwa .Kama inavyodhihirika , anaweza kulazimika hivi sasa kukalia viti vya upande wa upinzani.Tusubiri tuone Salvini atamlaumu nani.Yeye mwenyewe bila ya shaka hatojilaumu."

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Gakuba, Daniel