BREMEN : Ulaya yaunga mkono uhuru kwa Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 31.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BREMEN : Ulaya yaunga mkono uhuru kwa Kosovo

Umoja wa Ulaya umezitaka nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na Urusi kuunga mkono hatua za kutowa uhuru utakaosimamiwa kwa Kosovo.

Urusi ambayo ina uwezo wa kutumia kura ya turufu katika Baraza la Usalama inapinga kutolewa uhuru kwa Kosovo na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema hapo mapema kwamba mjumbe wa Umoja wa Mataifa Martti Ahtisaari atashindwa iwapo ataendelea kuushikilia mpango wake wa hivi sasa kwa jimbo hilo la Kosovo.

Duru za diplomasia zinasema wakati kukiwa na uungaji mkono mkubwa wa mpango huo kuna kutofautiana kidogo kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya juu ya Kosovo kupewa uhuru kutoka Serbia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Beremen Ujerumani amesema kwa vyo yvote vile uhuru kwa Kosovo ni muhimu kwa ajili ya utulivu wa eneo la Balkan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com