1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yaonesha makucha yake

Halima Nyanza(ZPR)4 Julai 2011

Na katika michuano ya kombe la dunia la soka la wanawake inayoendelea hapa Ujerumani, Brazil imeweza kuliongoza kundi D, baada ya jana kufanikiwa kuichabanga Norway mabao matatu kwa bila.

https://p.dw.com/p/11oMu
Wachezaji wa Brazil wakishangilia ushindiPicha: picture-alliance/dpa

Alikuwa ni Marta, mchezaji mahiri wa Brazil aliyeweza kuipatia timu yake ushindi huo, baada ya kufunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa bao jingine lililofungwa na Rozana.

Frauen-Fußball-WM 2011 Brasilien - Norwegen
Mchezaji mahiri wa Brazil, MartaPicha: dapd

Na hapo awali wawakilishi wa Afrika Guinea ya Ikweta ilishindwa kufurukuta mbele ya Australia, baada ya kuchabangwa mabao matatu kwa mbili.

Leo ni siku ya mapumziko kwa timu zote. Ambapo kesho timu nane zitajitupa uwanjani, New Zeland ikimenyana na Mexico, Uingereza na Japan.

Wenyeji Ujerumani watapambana na Ufaransa, Huku Nigeria wakikutana na Canada.