BRASILIA: Rais wa Ujerumani ziarani Brazil | Habari za Ulimwengu | DW | 07.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRASILIA: Rais wa Ujerumani ziarani Brazil

Rais Horst Köhler wa Ujerumani hii leo anaanza ziara ya siku tano nchini Brazil.Siku ya Alkhamisi atakutana na Rais mwenzake Luiz Inacio Lula da Silva mjini Brasilia.Kwa mujibu wa ofisi ya rais Lula,mada mojawapo itakayojadiliwa ni mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Nchi hizo mbili,pamoja na India na Japan zinagombea kuwa na viti vya kudumu katika Baraza la Usalama lenye usemi.Baada ya ziara yake nchini Brazil,Rais Köhler ataelekea Colombia.Ziara hii ya siku 12 barani Amerika ya Kusini,ilianzia nchini Paraguay,siku ya Jumatatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com