Bouba Diop afariki dunia | Michezo | DW | 30.11.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bouba Diop afariki dunia

Senegal na bara zima la Afrika linaomboleza kifo cha nyota wa zamani wa Senegal au Simba wa Teranga kama wanavyofahamika kwa jina la utani, Papa Bouba Diop. Diop alifariki hapo Jumapili akiwa na umri wa miaka 42.

Atakumbukwa sana kwa goli alilolifunga Senegal walipokuwa wakikwaana na mabingwa wa dunia wakati huo Ufaransa katika mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia ambapo miamba hao wa Afrika waliebuka kidedea.

Niederlage des Favoriten

Bouba Diop akifunga goli, Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa 2002

Alikuwa pia kwenye kile kikosi kilichopoteza fainali ya Kombe la Mataifa barani Afrika kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Cameroon.

Vyombo vya habari nchini Senegal vinasema kiungo huyo wa zamani amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.