1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Botswana yapiga kura katika mtihani kwa chama tawala

Bruce Amani
23 Oktoba 2019

Botswana inapiga kura katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kutoa ushindani wa kwanza halisi kwa chama tawala cha Botswana Democratic – BDP katika miongo yake mitano ya udhibiti wa taifa hilo

https://p.dw.com/p/3RlK3
Botsuana Parlamentswahlen
Picha: Getty Images/AFP/M. Bhuiyan

Chama kitakachoshinda kitahitajika kuuimarisha haraka uchumi, ambao tangu uhuru kutoka kwa Waingereza katika mwaka wa 1966 umekua kwa asilimia 8 kila mwaka na kuwa moja ya mataifa yenye mafanikio makubwa kabisa Afrika, lakini sasa linakabiliwa na kitisho kwa sababu ya kutegemea rasilimali moja kwa muda mrefu: almasi.

Huku akiahidi kuuimarisha uchumi wakati wa kampeni zake, Duma Boko, kiongozi wa chama cha Umbrella for Democratic Change, anatumai kukiondoa chama cha BDP cha Rais Mokgweetsi Masisi. Anaungwa mkono na rais wa zamani Ian Khama, ambaye alimkabidhi madaraka Masisi mwaka jana lakini sasa amejikuta katika mvutano mkali wa madaraka na rais huyo. Khama anamtuhumu Rais Masisi kuwa dikteta

Botsuana ehemaliger Präsident Khama Sereste
Rais wa zamani Ian Khama anaunga mkono chama cha upinzaniPicha: Getty Images/AFP/M. Bhuiyan

Kati ya idadi ya watu milioni 2.2 wa Botswana, watu 924,000 waliosajiliwa kupiga kura watawachagua wawakilishi 57 wa bunge la taifa na 490 wa serikali za mitaa. Mgombea wa chama kitakachoshinda kisha atakuwa rais mpya.

Masisi anajinadi kutokana na rekodi yake ya kupambana na rushwa, kama vile kufanya iwe lazima kwa maafisa wote wa sekta ya umma kutangaza mali zao, na kupunguza urasimu kwa biashara ndogondogo.

Khama, mtoto wa rais muanzilishi wa taifa hilo Seretse Khama, aligombana na Masisi kuhusu nyadhifa za uwaziri na hatua tata ya rais mpya ya kufuta marufuku ya uwindaji wa tembo mwezi Mei, ambayo Khama alikuwa ameitangaza miaka minne iliyotangulia. Ndovu hata hivyo hawajawa suala kuu katika kampeni hizi.

Wasiwasi mkuu kwa Wabotswana ni kiwango cha ukosefu wa ajira kuzungukia karibu na asilimia 20 na ukosefu mkubwa wa usawa licha ya hali ya ugavi sawa katika matumizi ya afya na elimu. Ili kupambana na hayo mshindi atahitaji kuchukua hatua Zaidi za kuutanua uchumi.

Uchimbaji wa Almasi umeshuka kwa moja juu ya tano ya Pato Jumla la Ndani katika mwaka wa 2018, ikilinganishwa na nusu katika miaka ya 1900, lakini bado inaunda robo tatu ya mapato ya fedha za kigeni, hata wakati sekta za benki na utalii zikinyakua sehemu kubwa ya mazao