1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bosi wa DFL awamwagia sifa mashabiki wa soka Ujerumani

Deo Kaji Makomba
22 Mei 2020

Awali kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda mashabiki wakakusanyika katika viwanja wakikiuka sheria inayoendelea ya kuwataka watu kutokukusanyika huku kukiwa na mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

https://p.dw.com/p/3cdi5
Deutschland Christian Seifert beim DFL-Neujahrsempfang in Frankfurt
Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya ligi kuu ya Ujerumani, DFL, Christian Seifert Picha: picture-alliance/dpa/A. Dedert

Wakati hekaheka za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga zikirejea tena tangu wikiendi iliyopita baada ya kusimama kwa muda kufuatia mlipuko wa virusi vya corona, Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya ligi kuu ya Ujerumani, DFL, Christian Seifert, amewamwagia sifa lukuki mashabiki wa soka nchini humu, kwa kukaa mbali na viwanja wikiendi iliyopita wakati wa mechi za Bundesliga zilipoanza tena.

Awali kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda mashabiki wakakusanyika katika viwanja wakikiuka sheria inayoendelea ya kuwataka watu kutokukusanyika huku kukiwa na mlipuko wa wa janga la virusi vya corona, kitendo ambacho kingeweza kuhatarisha juhudi za kukamilisha mechi za ligi ya Bundesliga bila kuwa na mashabiki uwanjani hadi mwishoni mwa mwezi Juni.

Lakini hakukuwa na matukio yoyote yaliyoripotiwa au kurekodiwa, na Seifert aliliambia gazeti la Sueddeutsche toleo la Ijumaa kwamba mashabiki walionyesha nidhamu jinsi inavyotawaliwa wakati huu.

"Tupo katika mazungumzo na taasisi kadhaa za mashabiki na ilikuwa wazi kwangu kwamba mashabiki hai katika eneo ni akili sana kuwapatia fadhila wakosoaji kwa kuandamana hadi viwanjani," alisema.

"Sikuwahi kuwa na shaka kuwa mashabiki watakuwa mfano wa kuigwa kila mahali." Mashabiki wamekuwa wakipingana na DFL katika miaka ya hivi karibuni na pia walikosoa kuanza tena kwa Bundesliga bila ya watazamaji.

Seifert alisema kuwa kila mmoja anapaswa kijuvuna kidogo kwamba licha ya tofauti zote jamii nzima ya mpira wa miguu imekubaliana kwa pamoja."

Afisa huyo alikiri bayana kuwa alikuwa na wasiwasi Jumamosi iliyopita kabla ya kuangalia kuanza tena kwa mechi badala ya kuungana na mke wake na mabinti zake katika matembezi ya kifamilia.

''Uko mbali na mchana mtulivu wenye burudani la kandanda. Hatimaye tulishangazwa, lakini hakuna anayeueleza kuwa mzuri sana. Utakuwa mzuri tena wakati watazamaji na mashabiki watakapokuwepo," alisema Seifert.

Maambukizi mapya ya Corona yagunduliwa klabu ya Dresden

Wakati hayo yakichomoza klabu ya soka ya Dynamo Dresden iliyoko ligi daraja la pili nchini Ujerumani, imesema kuwa mchezaji wao mwingine na mtu waliyekutana nae ambaye ni ofisa wa kitengo cha mazoezi walipimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona licha ya kikosi cha timu hiyo kuwa katika karantini kwa muda wa siku 14.

Fußball TSV 1860 München vs SG Dynamo Dresden - Fans von Dynamo Dresden
Mashabiki wa Dynamo Dresden.Picha: Imago Images/S. Kuttner

Vipimo hivyo vya virusi vya corona, vimefikisha idadi ya watu watano katika klabu hiyo ya Dresden na ikitoka katika kundi la tano la vipimo katika timu hiyo ya daraja la pili iliyopo katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi hiyo ya daraja la pili. Kwa wale waliopimwa mwanzoni na kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona sasa wamepimwa na kukutwa hawana maambukizi ya virusi hivyo, ilisema klabu hiyo na mazoezi kamili yataanza siku ya Jumamosi.

Mchezaji ambaye hivi karibuni alichukuliwa vipimo na kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, mmoja wa maofisa na watu waliokutana nao sasa wataingia katika kipindi zaidi cha karantini karantini. Mtu wa kwanza aliamriwa na mamlaka ya afya katika eneo hilo kuanzia Mei 9 baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo katika kuelekea kuanza kwa Bundesliga na ligi ya daraja la pili ya Ujerumani wikiendi iliyopita.

Mechi ya Dresden dhidi ya Hanover Jumapili iliyopita na zitakazofuata dhidi ya  Greuther Fuerth na ya ugenini dhidi ya vinara Arminia Bielefeld zote zimeahirishwa.

Kuanzia na mechi ya nyumbani dhidi ya VfB Stuttgart Mei 31 klabu ya Dresden iliyoko chini mwa msimamo wa ligi soka daraja la pili nchini Ujerumani itacheza mechi zote 9 zilizosalia katika msimu wao Juni 28 pamoja na mechi zao sita katika siku 15.

Bundesliga imekuwa ni ligi kubwa ya kwanza barani Ulaya kuanza tena kutimua vumbi mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya ligi hiyo kusimamishwa takriban miezi miwili iliyopita na hatua za usafi zilizotekelezwa kwenye mechi zote nchini kote Ujerumani.

Wachezaji wanapitia mara kwa mara vipimo vya virusi vya corona wakati mechi ikichezwa katika viwanja visivyokuwa na watazamaji kama sehemu ya miongozo madhubuti iliyopitishwa na serikali.

Ligi kuu na ligi ya daraja la pili hapa Ujerumani zitatoa heshima kwa wahanga wa janga la virusi vya corona katika kipindi cha mechi mbili zijazo. Zaidi ya watu 8,000 wamefariki dunia nchini Ujerumani ambayo imeripoti visa zaidi ya 175,000 vya Covid 19.

Vyanzo: (afp/dpa)