Borussia Mönchengladbach | Michezo | DW | 12.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Borussia Mönchengladbach

Borussia Mönchengladbach ikitamba miaka ya 1970 na ilikua miongoni mwa timu kali za Bundesliga pamoja na Bayern munich na FC Cologne.

Borussia Mönchengladbach,ni miongoni mwa timu zilizofanikiwa sana katika kabumbu la Ujerumani.Wameibuka mara 5 mabingwa, mara 3 washindi wa kombe la shirikisho la dimba na mara mbili mabingwa wa kombe la Ulaya la UEFA.

Borussia Mönchengladbach iliasisiwa August mosi,1900,lakini ilibidi kusubiri miaka 60 hadi kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ujerumani hapo 1960.Chini ya kocha maarufu marehemu Hennes Weisweiler,Borussia ilifaulu miaka 5 baadae kupanda daraja ya kwanza ya Bundesliga.

Kocha Weisweiler aliigeuza Borussia kuwa timu ya kushambulia na kuvunja mila za hapo kabla nah ii ilifanikiwa.Kocha wa baadae wa timu hii Horst Köppel anakumbusha:

“Hasa aleikuwa Günter Netzer,Juup Heynckes,Bernd Rupp,Herbert Laumen,chipukizi wa klabu hii pamoja na mimi ndio tuliochangia timu hii kujipatia jina kama hilo.”

Anakumbusha Horst Köppel, ambae 1968 alijiunga na klabu hii.Aliwasili wakati barabara kwani,miaka ya 1970ini,Borussia Mönchengladbach ndipo ilipotamba kabisa na kujipatia ushindi wake mkubwa kabisa katika historia yake.

Juni ,1971,Borussia Mönchengladbach ikawa timu ya kwanza katika historia ya Bundesliga kutetea taji lake.Na huo haukuwa mwisho,kwani nyota ya Borussia Mönchengladbach iliendelea kunawiri.

Miezi 4 baadae katika msimu wa 1971/72,Borussia iliichezesha Inter Milan ya Itali kindumbwendumbwe katika kombe la klabu bingwa barani Ulaya ilipoizaba mabao 7:1.

Halafu pakazuka mashtaka kwamba staid wa Inter Roberto Boninsegna alipigwa kopo la kinywaji kichwani uwanjani.iwapo kweli au la,Roberto alijitupa chini akigaragara .

Uwanjani wakati ule alikuwa pia kocha wa sasa wa timu ya taifa ya Nigeria-Super Eagles-Berti Vogts:

“Kopo lile lilivurumishwa sijui na nani,lakini liliamua hatima ya mchezo,kwavile ikaamuliwa na UEFA mchezo ule uchezwe tena.duru ya pili ikachezwa mjini Berlin.Hatukuweza kujipatia tena ushindi na tukapiogwa kumbo nje ya kombe hilo.”

Akumbusha Berti Vogts,aliewahi pia kuwa kocha wa Ujerumani.

Umaarufu wa B.Mönchengladbach,haukuingiwa na dosari kutokana na mkasa huo.Kinyume chake.Kwani, Borussia ikijihisi iko safu moja na hasimu yake mkubwa wakati ule-Bayern munich.1973,Borussia ikatwaa tena ubingwa wa Ujerumani.

Katika finali ya kombe la shirikisho inayokumbwa sana, Borussia Mönchengladbach iliilaza FC cologne mabao 2:1 mjini Düsseldorf baada ya kurefushwa mchezo.Alikua Günther Netzer alielifumania maridadi ajabu lango la Cologne kwa mkwaju mkali kabisa.

Hivi ndivyo mtangazaji alivyosimulia uwanjani finali hiyo:

“Hebu tuangalie nini Monchengladbach itafanya katika mashambulio haya yanayoendelea.Wanasonga mbele mpira akiwa nao Volker Danner,danner na mpirana amtupia Vogts nae ama Netzer.Netzer na mpira na autandika mkwaju m kali –ni bao.”

Baada ya bao hilo maridadi la ushindi,Günther Netzer aliaga Borussia Mönchengladbach na kujiunga na mabingwa mara kadhaa wa Spain na Ulaya, Real Madrid.Hii lakini, haikuizuwia Borussia kuendelea kutamba na kushinda.Ikiongozwa na kocha Hennes Weisweiler,Borussia Mönchengladbach ilitwaa kama timu ya kwanza ya Ujerumani kombe la ulaya la UEFA 1975.

Wiki 3 baadae, ikatawazwa Borussia pia mabingwa wa Ujerumani.Kocha Weisweiler akaiacha mkono Borussia baada ya kipindi cha miaka 11 na hatamu akashika kocha mwengine mashuhuri Udo Lattek.

Chini ya Lattek,Borussia ilitawazwa mabingwa mwaka uliofuatia 1976 na tena 1977 kabla hawakuvuliwa taji na FC Cologne, 1978.

Enzi za Borussia Mönchengladbach zikaanza kumalizika ingawa chini ya kocha bernd Krauss,Borussia ilitwaa kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani 1995 la kwsanza tangu 1979.

Baada ya hapo ikaanza kuyumbayumba na kama hasimu yake mkubwa wa miaka ya mwisho wa 1970 FC cologne, msimu ujao B.Mönchengladbach itacheza daraja ya pili ya Bundesliga na kama Cologne itajiwinda kurejea ghorofa ya juu ya Bundesliga.

 • Tarehe 12.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbj
 • Tarehe 12.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbj