1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Dortmund

Ramadhan Ali5 Julai 2007

Borussia Dortmund iliasisiwa 1909 na kabla kuanzishwa Bundesliga 1963 ilikwishatawazwa mabingwa mara si chini ya mara 3.

https://p.dw.com/p/CHbn

Borussia Dortmund ingawa iliasisiwa tayari 1909 ni baada ya vita vya pili vya dunia vilivyoishia 1945,ndipo klabu hii ilipoanza kutamba.Pale ilipoundwa Bundesliga-Ligi ya leo ya Ujerumani hapo 1963,Borussia Dortmund ilikwishatawazwa mabingwa wa ujerumani mara 3.

1965 Dortmund ilishinda kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani na ikakata tiketi ya kuania kombe la washindi la ulaya.Dortmund ikatia for a hadi finali hapo mei 1966 mjini Glasgfow dhidi ya Fc Liverpool ya Uingereza.Baada ya dakika 90 timu hizo 2 zilisimama suluhu bao 1:1.

Mpira ukarefushwa :

“Nafasi nyengine.Sigi,Sigi tia bao,ah, hakutia. Sasa lakini, mpira anao Libuda nae ana nafasi ya kutia bao-goal,goal,goal.Bao limenasa wavuni.”

Huo ukawa ushindi wa kwanza wa kombe la Ulaya kwa Borussia Dortmund na kwa timu yoyote ya Ujerumani.

Lakini ushindi huo ulifuiatiwa na kuteremka mlima kwa Dortmund:Mpango wa kuwapatia vijana nafasi katika timu hii na kuwapumzisha wakongwe,haukuifaidia.

Misukosuko ya Dortmund ilifikia kilele chake 1972 pale iliangukia daraja ya 3 ya kimkoa.1976,Borussia Dortmund ilirudi kuwa timu ya wastani katika Bundesliga. Mwishoni mwa msimu wa 1978 mahasimu 2-FC Cologne na Borussia Mönchengladbach zilikuwa kileleni hadi mechi ya mwisho ziokiania taji la ubimngwa.

Ili itawazwe bingwa na kuipiku FC Cologne,kwenye mechi ya mwisho, Borussia Mönchengladbach ilihitaji kuilaza B.Dortmund kwa mabao mengi sana.Hasimu wa Borussia Mönchengladbach, katika mpambano huo wa mwisho wa Ligi akawa B.Dortmund.Dortmund ikamuweka kijana chipukizi kulinda au kuliacha wazi lango lake.Kipa huyo chipukizi aliitwa Peter Endrulat.Ilipofika kipindi cha mapumziko Peter alikwishaokota mabao 6 wavuni na hivi ndivyo anavyokumbuka:

“Mawazo yangu yalikuwa kuendelea kucheza.Kwasababu nilijiambia haiwezekani katika kipindi cha pili mabao 6 zaidi yaingia wavuni.”

Katika kipindi cha pili mambo yalikuwa kama katika kipindi cha kwanza.Ni Borussia Mönchengladbach tu iliokua ikihujumu na wakaingiza 6 mengine.

Peter Endrulat anakumbusha:

“Wakishatia mabao 8 au 9,basi watakuwa wameshafikia mwisho wao.”

Wapi, Borussia Dortmund ilikomewa mabao 12 bila majibu.Lakini, hata mabao hayo 12 hayakuisaidia kitu Borussia Mönchengladbach kutawazwa mabingwa,lakini kwa kipa Peter Endrulat, huo ukawa mwisho wa maisha yake langoni.

Borussia Dortmund ilifufuka baada ya kunyakuwa ushindi wa kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani 1989 ilipoilaza Werder Bremen.Miaka iliofuatia hapo ndio ya mafanikio makubwsa katika historia ya klabu hii.1995 na 1996 B.Dortmund ilitawazwa kwa mara ya 4 na ya 5 mabingwa wa Ujerumani.

Katika msimu wa 1996/97 ulikua msimu tena wa kutamba katika champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya.Dortmund ilipambana na Juventus Turin katika finali na ikiongoza kwa mabao 2:1 katika uwanja wa Olimpik wa Munich:

“Stephane Chapuisat ndie anaebidi kutoka nje ya uwanja na kumpisha chipukizi Lars Ricken ambae amekweishawahi kutia mabao muhimu sana.Na sasa tubakie katika dimba,kwani Lars Ricken, autandika mkwaju mkali-shuti moja kali-goal.”

Ajabu kwani alipougusa tu mpira akiingia uwanjani,ametia bao.

Borussia Dortmund ikawa kileleni mwa dimba au alao bega kwa bega na Bayern Munich.

Mnamo miaka 2 iliopita,kwa juhudi kubwa klabu hii iliweza kuokolewa isifilisike.Kwani, mwaka 2000 ilikuwa klabu ya kwanza ya Ujerumani kushiriki katika soko la hisa.Mambo yakaiendea kombo.

Borussia Dortmund msimu uliopita, imekuwa bado ikipepesuka na jahazi lake likienda mrama.Iko mbali na 2001 ilipotamba mara ya mwisho na kutoroka na taji la ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya mwisho.