Borussia Dortmund wawaadhibu Freiburg | Michezo | DW | 05.10.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Borussia Dortmund wawaadhibu Freiburg

Borussia Dortmund walicheza na SC Freiburg na mshambuliaji wao Erling Haaland aling'ara sana katika mpambano huo alipocheka na wavu mara mbili na kusaidia kuunda goli moja pale timu yake ilipopata ushindi wa nne bila.

Chipukizi wa Dortmund Giovanni Reyna aliweka rekodi katika mechi hiyo kwa kusaidia kuunda magoli matatu.

Huyu hapa nahodha wa BVB Marco Reus.

"Vijana hawastahili kusoma magazeti badala yake fahamu zao waziweke kwenye mchezo na waendelee kufanya yale waliyoyafanya leo na tukifanya hivyo tutakuwa sawa. Vijana bado wanastahili muda wa kuendeleza yale waliyofanya leo kwa sababu mapambano yanaendelea kama nilivyosema," alisema Reus.