Borussia Dortmund hawakati tamaa | Michezo | DW | 22.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Borussia Dortmund hawakati tamaa

Borussia Dortmund walipata ushindi mkubwa wa magoli 4-0  siku ya Jumapili walipokuwa ugenini katika uwanja wa Schwarzwald Arena wakipambana na SC Freiburg.

Jadon sancho, Marco Reus, Mario Götze na Paco Alcacer ndio waliokuwa wafungaji wa mabao hayo. Kwa sasa Dortmund wanaishikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga wakiwa na pointi 69 pointi moja nyuma ya vinara Bayern Munich ambao wanawinda taji lao la saba huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee.

Mechi nyengine ya Bundesliga jana ilishuhudia Hannover 96 kutoka sare ya kutofungana na Hertha Berlin. Hii leo VfL Wolfsburg watakuwa wanawakaribisha Eintracht Frankfurt.