BOMU LAUA 2 IRAK | Habari za Ulimwengu | DW | 24.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BOMU LAUA 2 IRAK

BAGHDAD:

Bomu la motokaa la mtu aliejiripua lililengwa kituo cha polisi katika wilaya ya Dora mjini Baghdad leo na kuwaua polisi 2 na kuwajeruhi wengine 7. Mripuko huo ulinguruma kama radi katika shina la mji mkuu Baghdad na kupaza wingu kubwa la moshi angani.

Taarifa nyengine kutoka Baghdad yasema serikali ya Irak imewatia kizuizini walinzi wa makamo-waziri mkuu Salam al-Zubayi ili kuwahoji baada ya mjumbe huyo wa hadhi ya juu wa ki-suni serikalini kujeruhiwa katika hujuma ya bomu hapo jana.

Na taarifa iliochapishwa kwa niaba ya waasi wa ki-suni wanaoongozwa na tawi la Irak la al Qaeda, imesema ni kikundi hicho kilichoripua mabomu 2 yaliomjeruhi makamo-waziri mkuu Salam al-Zubayi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com