Bolt ambwaga Gatlin katika fainali ya mita 200 | Michezo | DW | 28.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bolt ambwaga Gatlin katika fainali ya mita 200

Mwanariadha wa mbio za kasi Mjamaica Usain Bolt, ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Beijing, China. Mrakenai Justin Gatlin alimaliza wa pili

Bolt alitimuka mbio hizo katika muda wa sekunde 19.55 na kuinyakulia nchi yake nishani nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha wa kasi zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi mwaka huu.

Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo na wa nne mfululizo katika mbio hizo za dunia. Mmarekani Justin Gatlin, alimaliza wa pili na kushinda medali ya fedha sawa tu na ilivyokuwa katika mbio za mita mia moja. Gatlin alitumia muda wa sekunde 19.74.

Katika fainali za mita mia nne kwa kina dada Felix Allyson wa Marekani alinyakuwa medali ya dhahabu, huku Shaunae Miller wa Bahamas akipata ya fedha. Shericka Jackson wa Jamaica alichukua shaba

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef