1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolt aangazia macho Michezo ya Olimpiki Rio

18 Aprili 2015

Mwanariadha wa kasi zaidi ulimwenguni, Mjamaica Usain Bolt amesisitiza kuwa macho yake yanaangazia Mashindano ya Olimpiki ya Rio mwaka ujao, huku rekodi mpya ya ulimwengu katika mbio za mita 200 ikiwa lengo kuu

https://p.dw.com/p/1FASN
Leichtathletik-WM Moskau
Picha: picture-alliance/dpa

Bolt ni bingwa mara sita wa Olimpiki, kwa kushinda mbio za mita 100 na 200 mjini Beijing mwaka wa 2008 na London miaka minne baadaye, wakati pia akinyakua medali mbili za dhahabu kama sehemu ya kikosi cha Jamaica kinachotawala ulimwengu katika mbio za masafa mafupi za mita mia moja wanariadha wanne kupokezana vijiti. Pia anashikilia rekodi za ulimwengu za mita mia moja na mia mbili.

Bolt, ambaye atastaafu mwaka wa 2017 baada ya mashindano ya ubingwa wa ulimwengu, ambapo atashiriki tu katika mbio za mita mia moja, atakimbia kesho mbio za maonesho za mita 100 mjini Rio. Rekodi yake ya mbio za mita 100 ni sekunde 9.58 wakati ile ya mita mia mbili ikiwa 19.19

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu