1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bodi ya magavana ya shirika la IAEA kujadiliana kuhusu Iran

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAGJ

VIENNA

Magavana wa bodi ya shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nulikia IAEA wamepanga kukutana jumatatu katika kikao maalum ambacho kinatazamiwa kugubikwa na mjadala kuhusu ripoti inayoeleza juu ya kukataa kwa Iran kuweka wazi shughuli zake za kinuklia.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya mkuu wa shirika hilo la IAEA Mohammed Albaradei,Iran bado inatakiwa kutoa maelezo kamili yatakayounga mkono hoja yake kwamba mradi wake wa Kinuklia haulengi kutengeneza bomu la Nuklia kama inavyodaiwa na mataifa ya nchi za magharibi.

Aidha ripoti hiyo inasema kwamba Iran inaendelea na shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium licha ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuitaka nchi hiyo kukomesha mpango wake huo.