1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobi Wine ashinda kesi ya kutaka kukifuta chama chake

Iddi Ssessanga
21 Oktoba 2020

Mahakama kuu nchini Uganda umempa ushindi Robert Kyagulanyi, aka Bobi Wine, katika kesi ya kupinga uhalali wake kuongoza chama cha National Unity Plaftform NUP. Mahakama imewaamuru walalamikaji kumlipa fidia Bobi Wine.

https://p.dw.com/p/3kF1p
Robert Kyagulanyi
Picha: Emmanuel Lubega/DW

Wagombea walioteuliwa kuwania kwa tiketi ya chama cha National Unity Platform, NUP, wanaweza sasa kuvuta pumzi baada ya mahakama kuu mjini Kampala kutupilia mbali kesi iliyopinga kusajiliwa kwa chama hicho na kubdilishwa jina kutoka National Unity Reconciliation and Development Party, NURP.

Soma pia: Bobi Wine ashtakiwa kwa Uhaini

Jaji Musa Ssekaana, pia amemwaamuru rais wa zamani mwasisisi wa chama hicho Moses Kibalama Nkonge na Katibu Mkuu Paul Ssimbwa Kagombe kulipa gharama kwa kiongozi wa NUP ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyipamoja na wengine watano kwa kuburutwa mahakamano isivyo halali.

Robert Kyagulanyi
Bobi Wine akizzungumza na wafuasi wake baada ya kushinda kesi mahakama kuu mjini Kampala, Oktoba 21, 2020.Picha: Emmanuel Lubega/DW

Jaji Ssekaana alitumia mamlaka yake kumuongezea Kibalama na Kagombe kama walalamikaji katika kesi hiyo baada ya wawili hao kujirudi kwenye kiapo chao katika ushahidi mbele ya mahakama baada ya kushindwa kupata kiasi cha dola milioni 5 walizoahidiwa.

Soma pia: Wafuasi wa Bobi Wine kufikishwa katika mahakama ya kijeshi

Jaji pia ameshikilia kwamba walalamikaji walipaswa kuomba mapitio ya kisheria ndani ya muda wa miezi mitatu baada ya mbadiliko ya jina la chama kutoka NURP kwenda NUP, hiyo ndiyo kusema kufikia Juni 6, 2019 lakini badala yake walifungua shauri Agosti 24, 2020, baada ya kupita zaidi ya mwaka mmoja.

"Ombi lilifanywa kwa mtazamo wa kujiptia pesa wakati huu wa msimu wa uchaguzi na waombaji hawana malalamiko halali lakini walitafuta tu kuonekana na kujipatia pesa za haraka," alisema jaji.

"Mahakama imewezeshwa kukataa msaada na kuwanyima haki ya kupata mapitio ya kisheria kwa kuzingatia msuala kadhaa, kwa mfano, haipendezi kuruhusu madai yaliopitwa n wakati kushughulikiwa na mahakama, kunapswa kuwa na hitimisho la usuluhishi," aliongeza Jaji Ssekaana.

Uganda Pop Star l MP Robert Kyagulanyi, alias Bobi Wine
Bobi akitoa ishara wakati alipozuru mji wa Nairobi, Oktoba 12, 2019.Picha: picture alliance/AP Photo/B. Inganga

Malalamiko ya upande wa mashtaka

Uongozi wa Kyagulanyi katika chama cha NUP ulikuja chini ya uchunguzi baada ya wawili kati ya waasisi wake, Difas Basile na Hassan Twala, kufungua shauri mahakama kuu wakisema Kibalama, rais mwasisi, alibadili jina la chama na kuhamisha uongozi wake kwa Kyagulanyi na kundi lake bila taarifa na ridhaa yao.

Soma pia:Mkakati wa kukifuta chama cha Bobi Wine wapelekwa mahakamani 

Bobi Wine alishtakiwa kwa pamoja na Tume ya Uchaguzi, EC, Mwanasheria Mkuu, Kaimu Rais wa Chama cha National Unity Reconciliation Party, NURP, Kibalama, viongozi wa chama cha National Untiy Party NUP, David Lewis Rubongoya, Aisha Kabanda, Joel Ssenyonyi, Flavia Kalule Nabagabe, Fred Nyanzi Ssentamu na Paul Ssimbwa Kagombe.

Bobi Wine aeleza nia ya kuwania urais nchini Uganda

Walalamikaji walidai kuwa NURP ilitangazwa kwenye gazeti la serikali kama chama cha siasa nchini Uganda Desemba 13, 2004, na kupewa cheti cha usajili Desemba 28, 2004.

Wakaeleza zaidi kwamba mwaka 2019, bila haki yoyote na katika ukiukaji wa katiba ya chama, bwana Kibalama, na tume ya uchaguzi walibadilisha kinyume cha sheria jina la chama hicho hadi NUP na Julai 14, 2020 alikabidhi uongozi wa chama kwa Kyagulanyi na Kagombe.